Mpanda FM

Katavi yaongoza kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi nchini Tanzania

20 December 2023, 4:43 pm

Muwakilishi kutoka katika ofisi ya takwimu ya taifa NBS Lusy Minja akizungumza na viongozi, watendaji na wadau katika kikao Cha mafunzo ya usambazaji na matumizi ya Matokeo ya sensa ya watu na makazi. Picha na Festo Kinyogoto

Viongozi,watendaji na wadau mkoani Katavi wameaswa kuyatumia vizuri Matokeo ya sensa ya sita ya watu na makazi iliofanyika mwaka 2022 katika kutimiza adhma ya serikali

Na Festo Kinyogoto – Katavi

Mkoa wa Katavi  unaongoza Kwa kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi nchini Tanzania

Viongozi,watendaji na wadau mkoani Katavi wameaswa kuyatumia vizuri Matokeo ya sensa ya sita ya watu na makazi iliofanyika mwaka 2022 katika kutimiza adhma ya serikali ya kutekeleza shughuli  za kimaendeleo.

Hayo yamesemwa na mgeni rasmi Onesmo Buswelu akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko  katika kikao Cha mafunzo ya usambazaji na matumizi ya Matokeo ya sensa ya watu na makazi Kwa viongozi, watendaji na wadau mkoani  Katavi ambapo amesema Matokeo hayo ndio Muongozo sahihi wa shughuli zote zinazotakiwa kutekelezwa.

Sauti ya Onesmo Buswelu

Muwakilishi kutoka katika ofisi ya takwimu ya taifa NBS Lusy Minja amesema mkoa wa Katavi  umeongoza Kwa kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi nchini Tanzania, hivyo mipango lazima iakisi ongezeko la watu ili kukidhi idadi na ustawi wa Maisha ya wananchi.

Sauti ya Lusy Minja

 Aidha Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa mkoa wa pili Kwa idadi kubwa ya watoto ikiwa na asilimia 56 nyumaa ya Simiyu yenye asilimia 57.

Sauti ya Mratibu

Kikao hicho kimelenga kutumia takwimu za ongezeko Hilo katika kuendana na kasi ya ongezeko la watu Kwa mujibu wa takwimu katika huduma zote za kijamii, uchumi,afya umeme, maji, elimu siasa na utamaduni huku kuzaliana uhamiaji na Hali ya kiuchumi zikitajwa kama sababu za ongezeko Hilo.