Mpanda FM

TAKUKURU Katavi yajipanga uchaguzi serikali za mitaa

9 February 2024, 2:16 pm

Tumejipanga kutoa elimu na kuzuia rushwa  kwa Wananchi na wagombea Ili kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa  unakuwa huru na haki kwa mwaka huu na Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.Picha na mtandao

Na Samweli Mbhugi-Katavi

Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa TAKUKURU mkoa wa Katavi Imesema wamejipanga  kikamilifu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.

Akizungumza na Mpanda Radio fm afisa wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Felicion Katininda amesema wamejipanga kutoa elimu na kuzuia rushwa  kwa Wananchi na wagombea Ili kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa  unakuwa huru na haki kwa mwaka huu na Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Sauti ya afisa wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Felicion Katininda akizungumza kuhusu kutoa elimu kwa wananchi na wagombea.

Pia amesema kuna wagombea huwa wanatoa takrima kwa wananchi kitu ambacho hakitofautia na rushwa, hivyo katika kipindi chote cha maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hakitaruhusiwa.

Felicion Katininda amewatoa hofu wanachi wasiogope kutoa taarifa kwani kuna sheria inayomlinda mtoa tarifa pindi atakapo toa tarifa za rushwa katika ofisi za TAKUKURU.

Sauti ya afisa wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Felicion Katininda

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi watakaopata nafasi ya kugombea kuwa makini kuto kutoa rushwa au kupokea rushwa kwani ni wajibu wa kila mtu kuzuia rushwa.