Mpanda FM

Wanachama wa Yanga Mpanda Wafanya Matendo ya Huruma

26 July 2023, 5:50 pm

KATAVI

Baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga Mkoa wa Katavi wamefanya matendo ya huruma katika kilele cha wiki ya wananchi kwa kuchangia damu na kutoa msaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima.

Wakizungumza na Mpanda radio Fm wamesema uchangiaji wa damu utasaidia kuokoa maisha ya watu wengi wenye uhitaji wa damu.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi Boniface Limo amewashukuru wanachama na mashabiki wa yanga kwa kujitoa kuchangia damu huku msimamizi wa kitengo cha damu salama katika hospital hiyo Neema Chipalo pamoja na kuwashukuru wanayanga ameeleza kiasi cha damu kilichopatikana mara baada ya zoezi hilo.

Kwa upande wake mlezi msaidizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nsemlwa sister Pascalia Ntasima amewashukuru wanayanga kwa kuwatembelea na kutoa msaada kwa watoto hao.

#mpandaradiofm97.0

#yangasc