Mpanda FM
Mpanda FM
29 June 2026, 3:13 pm

“Kumekuwa na mbwa wanaodhurura ovyo hawana uangalizi kutoka kwa wamiliki hali inayozua hofu “
Na Anna Milanzi- Katavi
Wakazi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamewasisitiza wamiliki wa mbwa kufungia mbwa wao ili kuwaepusha na ugonjwa wa kichaa cha mbwa ambao mtu anaupata baada ya kung’atwa na mbwa mwenye maambukizi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao akiwemo Happynes Samwel, Nicolaus Luwele, Sesilia Sangu wamesema kuwa kumekuwa na mbwa wanaodhurura ovyo hawana uangalizi kutoka kwa wamiliki hali inayozua hofu kwa wakazi hao hasa kupata kichaa cha mbwa endapo mtu kang’atwa na mbwa mwenye maambukizi.
Daktari wa mifugo wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Eward Mtega ameeleza visa vilivyoripotiwa vya watu waliong’atwa na mbwa.
Amesema zipo hatua wanazozichukua endapo wakipata taarifa za mtu kung’atwa na mbwa.
Mratibu wa huduma za matibabu hospitali ya manispaa ya Mpanda Daktari Mundhiri Bashiri amewataka wananchi wanaong’atwa na mbwa kufika haraka katika kituo cha kutolea huduma za afya ili waweze kupatiwa matibabu.
Hata hivyo wamiliki wa mbwa wamekumbushwa kuwafungia mbwa wao na kuwapatia chanjo ili kudhibiti madhara kwa binadamu .