Mpanda FM

Wadau wa nyama 30 watozwa faini Katavi

16 June 2023, 7:11 pm

KATAVI.

Zaidi ya shilingi milioni 3 zimetozwa kwa wadau wa nyama 30 kati ya 81 baada ya kupigwa faini kwa makosa kama ubovu wa miundombinu katika machinjio mkoani Katavi.

Akizungumza na Mpanda Redio FM Afisa mfawidhi wa nyama kanda ya Magharibi Joseph Kulwa amesema kuwa wamefikia hatua hiyo Baada ya zoezi la ukaguzi kwa wadau wa nyama ambapo ukaguzi umefanyika katika halmashauri ya Mpanda na Mpimbwe na kubaini kutokuwepo kwa vyoo katika machinjio ya mifugo pamoja na uchafu wa mazingira ya kuuzia nyama .

Kwa upande wa baadhi ya wananchi mkoani Katavi wametoa maoni ambapo wameshauri kufanyika kwa usafi katika maeneo ya machinjio na bucha ili kuweza kumlinda mlaji kutopatwa na magonjwa.

#mpandaradiofm97.0

#katavists