Mpanda FM

Bado wazazi wana wajibu wa kuibua vipaji vya watoto wao.

4 March 2023, 5:27 pm

KATAVI

Baadhi ya wazazi mkoani katavi wamesema wanao wajibu wa kuwapa nafasi watoto kushiriki katika michezo ili kuibua vipaji walivyo navyo watoto na kuviendeleza ili viweze kuwa msaada kwa maisha ya baadae ya mtoto.

Wakizungumza na mpanda redio fm wamesema ni jukumu Lao kuwatengea muda wa kushiriki katika michezo baada ya masomo na kuwanunulia vifaa vya michezo ili watoto waweze kuibua vipaji walivyo navyo huku wakiomba serikali kuboresha miondombinu ya michezo mashuleni .

Afisa michezo mkoa wa Katavi Karoli Steven amewataka wazazi walezi na walimu kuendelea kuwapa nafasi watoto kushiriki katika michezo huku akiwaomba wawakilishi wa mkoa wa Katavi katika mashindano mbali mbali kufanya vizuri ili kuhamasisha na wengine kujiunga kwenye michezo.