Mpanda FM

Sauti ya Katavi (Matukio)

7 June 2023, 10:54 am

KATAVI

Watu wawili  Mkoani Katavi wamehukumiwa kifungo cha Miaka Mitatu kila mmoja jela kwa tuhuma za kuua bila kukusudia huku wengine Wanne wakienda Jela kwa makosa ya Wizi.

Mwandishi wa Mpanda Radio Henry Mwakifuna amefika ofisi za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi  Ali Makame Hamad na kutuandalia Taarifa ifuatayo;

KATAVI

Maafisa tarafa na watendaji wa kata wa mkoa wa Katavi wametakiwa kutekeleza majukumu ya serikali katika maeneo yao ya kazi..

Agizo hilo limetolewa wakati walipokuwa wakipata mafunzo mkoani hapa, huku Jumla ya watendaji wa kata 60 na maafisa tarafa 9 mkoani hapa wamepata mafunzo.na Mwandishi wetu GLADNESS RICHARD Anakuja na undani wa taarifa hiyo.

MPANDA

kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu tanzania ya mwaka 2022 (LHRC) haki ya kutofanyiwa ukatili ni miongoni mwa haki za binadamu zilizokiukwa zaidi hivyo kupelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kimwili katika jamii

mwandishi wetu LUSY DASHUD amefanya mahojiano na mkurugenzi wa shirika la paralegal ya mkombozi fujensia kapama ili kutufahamisha zaidi juu ya wajibu wa watu wa karibu katika kuzuia ukatili

DODOMA-KATAVI

Serikali imesema kuwa kupitia TBS na Sido imetenga fedha kwa ajili ya kwenda kuwafundisha wajasiliamali wanatengeneza pombe za kienyeji ili kuzipa thamani pombe hizo kwa kuwa serikali inatambua mchango wake katika kutengeneza kipatokwa wanaofanya shughuli hizo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa uwekezaji,Viwanda nanBiashara Mhe. Exaud Kigahe wakati akijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe aliyetaka kujua Serikali inamkakati Gani wa kuongeza Kodi kwenye pombe zote kutoka nje ili kuzipa thamani pombe za ndani na swali la pili je Serikali imeshaanza kuzipatia leseni pombe ambazo walizipiga marufuku kama vile gongo.

Kufuatia hilo suti ya Katavi imewatafuta wantu wanaijishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa pombe za kienyeji je wanamaoni gani kuhusiana na hilo.

Mandishi wetu KINYOOTO  FESTO anakuja na undani wa taarifa hii.