Mpanda FM

Mafunzo uongozi yatolewa Katavi

7 June 2023, 10:59 am

KATAVI

Maafisa tarafa na watendaji wa kata mkoa wa Katavi wametakiwa kutekeleza majukumu ya serikali katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi wakati wa utolewaji wa mafunzo ya uongozi kwa maafisa tarafa na watendaji wa kata zote mkoani hapa ambapo amesema serikali itaendelea kuwawezesha ili kufanya kazi katika mazingira rafiki.

Naibu mkuu wa chuo cha serikali za mitaa Michael Msendekwa ambaye ni moja ya watoa mafunzo hayo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuboresha utendaji kazi wa viongozi hao katika maeneo yao.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru kwa kupata mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi katika maeneo yao ya kazi.

Jumla ya watendaji wa kata 60 na maafisa tarafa 9 mkoani hapa wamepata mafunzo hayo.

#mpandaradiofm97.0

#katavists

#wizarayatamisemi