Mpanda FM

Katavi watakiwa kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto

10 October 2024, 4:18 pm

Wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ametoa maoni  mseto kuhusiana na sababu zinazopelekea wazazi na walezi kuwafanyia ukatili watoto wao.

Wakizungumza na Mpanda Radio FM wananchi hao wamesema kuwa ukosefu wa elimu na malezi duni imekuwa ni sababu kubwa zinazopelekea watoto kufanyiwa ukatili

Sauti za wananchi wakizungumza

Nae mkaguzi wa polisi Judith Mbukwa ambaye ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa katavi  amethibitisha kuwa wazazi wengi wamekuwa wakiwafanyia ukatili watoto wao kutokana na imani za kishirikina pamoja na umaskini hivyo amewasihi wazazi kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi katika kutokomeza ukatili dhidi ya watoto

Sauti ya mkaguzi wa polisi Judith Mbukwa ambaye ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto Katavi akizungumza

Ikumbukwe kuwa sheria ya mtoto inazuia mtoto kufanyiwa ukatili, unyama pamoja na vitendo visivyo vya kibinadamu au udhalilishwaji unaohusisha matendo ya kimila yanayoondoa utu wa mtu au kuathiri ustawi wa akili na maumbile yake.