Mpanda FM

Maoni ya Machinga juu ya Fedha za Ujenzi wa Ofisi kila Mkoa

20/10/2022, 11:40 AM

MPANDA

Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga Mkoani Katavi wamekuwa na maoni tofauti tofauti baada ya Serikali kutenga kiasi cha shilingi milion 10 za ujenzi wa ofisi za machinga kila Mkoa.

Wakizungumza na Mpanda radio fm wafanyabiashara hao wamesema ujenzi wa ofisi za machinga kila mkoa uendane na masharti rafiki yatakayo wasaidia kufanya biashara huru.

Kwa upande wake mwenyekiti wa machinga  Mkoani Katavi Marko Erenest amesema tayari fedha hiyo imekwisha  tengwa katika bageti mpya ya serikali  ya mwaka 2022/2023 huku akisisitiza kuwa itaenda kuwa na manufaa kwa wafanyabiashara hao.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika Ziara mkoani kagera amesema serikali imetenga shilling million 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za machinga kila mkoa Nchini huku akiwaagiza wakuu wa mikoa kuwatafutia maeneo.