Mpanda FM

Waliofyekewa mahindi Katavi washukuru mchango wa Mpanda Radio FM

18 March 2024, 2:08 pm

Wakulima hao walifyekewa mahindi baada ya kile kilichosemwa ni ukiukwaji wa sheria ya kulima mazao marefu kwa Manispaa ya Mpanda katika maeneo yaliyokatazwa, lakini yaliacha maswali baada ya kadhia hiyo kuwakumba wakulima watatu pekee huku maeneo mengine mazao yakiendelea kuachwa

Baada ya kituo cha matangazo Mpanda Radio Fm kufuatilia sakata la Wananchi kufyekewa mahindi kata ya Mpanda hoteli manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa shukrani katika walaka ulioandikwa kwenda kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Ndugu Joseph Lwamba, kwa hatua za kushughulikia fidia walioamuliwa kulipwa na katibu Mwenezi wa CCM Ndugu Paul Makonda katika ziara yake mkoani Katavi.

Walaka huo kwenda kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Ndugu Joseph Lwamba umebebwa na kichwa cha habari kilichosomeka YAH: SHUKRANI NA KUKUPONGEZA KWA KAZI NZURI UNAYOFANYA YA KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI NA HASA MGOGORO WETU WA KUFYEKEWA MAHINDI NA VIONGOZI WA KATA YA MPANDA HOTEL TAREHE 23/12/2023.

Muonekano wa mbele pamoja na kichwa cha habari cha walaka wa wakulima hao uliopelekwa kwa mweyekiti wa CC wilaya ya Mpanda.

Wakulima hao walifyekewa Mahindi baadaya ya kile kilichosemwa ni ukiukwaji wa sheria ya kulima mazao Marefu kwa Manispaa ya Mpanda katika maeneo yaliyokatazwa, lakini yaliacha maswali baada ya kadhia hiyo kuwakumba wakulima watatu pekee huku maeneo mengine mazao yakiendelea kuachwa.

Jambo lililoibua taharuki kwa wakazi wa mpanda na Tanzania kwa ujumla na ndipo waziri wa kilimo Mhe HUSSEN BASHE aliwasiliana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda ndugu Hidary Summry kusitisha zoezi hilo.

Mpanda Radio fm ilifuatilia suala hili kwa kuandika hanbari kusikiliza pande zote mbili za waathirika wa kadhia hiyo pamoja na viongozi wa Manispaa ya Mpanda akiwemo Mkuu wa wilaya Mhe, Jamila Yusuph na alinukuliwa akisema kufyeka mazao yaliyokuwa sio swa na watakaa pamoja na waathirika waangalie namna ya kuwafuta maumivu bila kutaja maumivu hayo yatafutwa kwa njia gani.

Moja ya shamba lililofyekwa mahindi la mkulima Nestory Kameme wakati Jeshi la mgambo likiendelea na kazi hiyo Tarehe 13 december 2023. Picha na Festo Kinyogoto

Kufuatia hatua zote za Mgogoro huo Mpanda Fm ilisimama na pande zote kuhakikisha umma wa watanzania na wanakatavi unafahamu Kuhusu sakata hilo Mpaka ilipofika hatima ya kuamuliwa katika mkutano wa hadhara wa katibu wa itikatdi na uenezi CCM taifa Paul Makonda kuwaamuru wilaya ya Mpanda kulipa fidia kwa wakulima hao ambapo wameshukuru kituo hiki kwa hatua zote za kuwakutanisha na wahusika na kuufahamisha umma.

Huu ni ukurasa wa nne wa walaka huo ambapo katika nambari 11 ya mambo yaliyoorozeshwa ndipo shukrani kwa Mpanda Radio Fm zimetajwa.

Uongozi wa Mpanda Radio Fm umezipokea shukrani hizo na itaendelea kufanya kazi kwa weledi bila kuegemea upande wowote ili kuhakikisha Wananchi na viongozi wanaendelea kushirikiana ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa mkoa wa katavi na taifa kwa ujumla.

SISI NI SAUTI YA KATAVI