Mpanda FM

Mazishi ya aliyekuwa mmiliki wa Mpanda Fm kufanyika April 22, 2024

21 April 2024, 3:48 pm

Pichani ni aliyekuwa mmiliki wa kituo cha mpanda redio fm Aleem Kanji enzi za uhai wake

“Kifo chake kimetokana na ajali ambapo mara baada ya kufikishwa hospital kwa ajili ya matibabu alifariki dunia”

Na Betold Chove- Katavi

Mkurugenzi wa Mpanda radio fm Amin Mitha Ametangaza kifo cha mmiliki wa Kituo cha kurushia matangazo cha Mpanda [Mpanda radio fm 97.0] Aleem Kanji  kilichotokea nchini Zambia alikokua akiishi.

Akitoa taarifa kwa umma Mitha amesema kifo hicho kimetokea tarehe 19 nchini Zambia kutokana na ajali na amefariki dunia mara baada ya kufikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu

Sauti ya Amin Mitha akitangaza kutokea kwa kifo hicho

Aidha Mitha amewaomba wasikilizaji wa  Mpanda radio fm, ndugu, jamaa na marafiki  kuwa watulivu wakati taratibu za mazishi zikiwa zinaendelea.

Sauti ya Amin Mitha akieleza kuhusu utaratibu wa mazishi utakavyokuwa

Mazishi ya mmiliki wa Mpanda radio fm Aleem Kanji yanatarajiwa kufanyika April 22, 2024 jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Ismailia Kijitonyama nyuma ya Millenium Tower.