Mpanda FM

Makundi ya kihalifu na utelekezaji wa watoto

28 September 2023, 6:26 am

Picha na Mtandao

Utelekezaji wa watoto katika familia inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea ukosefu wa elimu kwa vijana na kuongezeka kwa makundi ya kihalifu Katavi.

Na Ben Gadau – Mpanda
Utelekezaji wa watoto katika familia inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea ukosefu wa elimu kwa vijana na kuongezeka kwa makundi ya kihalifu katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Wananchi watoa taarifa za watoto walio telekezwa katika ofisi za serikali ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.

Wakizungumza na Mpanda Redio Fm baadhi ya wananchi wametoa maoni mseto na kueleza familia ikitelekezwa inachangia ukosefu wa elimu kwa vijana huku wakihusisha na ongezeko la watoto wa mitaani linalopelekea makundi ya kihalifu.

Sauti za wananchi

Hadija Kipingu ni Afisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Mpanda amewataka wananchi kutoa taarifa za watoto walio telekezwa katika ofisi za serikali ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.

Sauti ya Afisa ustawi Khadija Kipingu

Kwa mujibu wa Sheria ya mtoto Na.21 ya mwaka 2009 imelenga kuimarisha ulinzi, matunzo na haki za Watoto Tanzania bara pia sheria hiyo imeanisha haki ya mtoto kulelewa na wazazi wake na haki ya kupata mahitaji ya msingi ikiwemo chakula,malazi,mavazi, matibabu,chanjo,elimu,Pamoja na haki ya kucheza na kuburudika