Mpanda FM

Mpanda: Uchimbaji madini uzingatie maeneo tengefu

30 June 2023, 10:21 am

MPANDA

Wananchi wa kijiji cha Dirifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kutunza mazingira na kufanya shughuli za uchimbaji madini kwenye maeneo yaliyotengwa.

Hayo yamesema na mtendaji wa kijiji hicho Evelius Mathayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara baada ya kuona wananchi wakiendelea na shughuli za kuchimba mashimbo kwenye maeneo ya makaburi jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Kwa upande wa wananchi wa kijiji hicho wakizungumza na Mpanda Radio Fm wamekumbusha wachimbaji kufuata sheria kwa kuchimba maeneo tengefu huku wakipaswa kutoa heshima kwa miili iliyopumzishwa kwenye makaburi hayo.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayamadini