Mpanda FM
Mpanda FM
27 June 2026, 6:13 pm

“ Lengo la kufanya hivyo ni kuchangia kuuweka mkoa katika hali ya usafi“
Na Anna Milanzi -Katavi
Katika kuendelea na maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ,TRA mkoa wa Katavi imekuja na suluhisho la uhifadhi wa taka na kuweka hamasa ya usafi wa mazingira.

Akizungumza katika uwanja wa azimio mara baada ya kukamilika kwa matembezi ya kilometa 5 kaimu meneja wa TRA mkoa wa Katavi Joshua Mile amesema lengo la kufanya hivyo ni kuchangia kuuweka mkoa katika hali ya usafi huku akieleza mapipa zaidi ya 25 yanatarajiwa kuwekwa katika maeneo ya mji wa Mpanda.
Akimwakilisha mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli, Gwalusajo Kapande amesema mapipa ya taka yatasaidia kuweka mji safi ambapo amewasisitiza wananchi pia kulipa kodi ili kuleta maendeleo
Katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela amesema TRA imepiga hatua katika ukusanyaji wa mapato kwa kuvuka malengo waliyojiwekea.
Nao baadhi ya wananchi akiwemo Khadija Mtalika na Izack Joseph waliohudhuria matembezi hayo wamepongeza kazi zinazofanywa na mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA )na kusisitiza wananchi wengine kulipa kodi.
Miongo mitatu ya TRA Katavi, jamii inaendelea kupata elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi.