Katavi: Mwenyekiti CHADEMA awataka wanachama wa chama hicho kutokubali kuchukuliwa kizembe
9 September 2024, 7:30 pm
Mwenyekiti chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake .picha na John mwasomola
“kutokana na matukio yanayojitokeza ya watu kutekwa na kuuawa wanatakiwa kujilinda na kutokubali kuchukuliwa“
Na John Mwasomola -Katavi
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mkoani Katavi amewataka wanachama wa chama hicho kuwa makini wawapo katika majukumu yao na kujilinda
Mwenyekiti wa CHADEMA Rhoda Kunchela ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake, ambapo amesema kuwa kutokana na matukio yanayojitokeza ya watu kutekwa na kuuawa wanatakiwa kujilinda na kutokubali kuchukuliwa.
Sauti ya mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa katavi akizungumza
Mbali na hayo pia amewataka wananchi ndani ya mkoa wa Katavi kujitokeza kushiriki katika zoezo la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi november mwaka huu.
Pia amewahakikishia wananchi na wagombea wote wa chama hicho kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni huru na haki hivyo wasiogope kuchagua viongozi ambao wanafaa kushughulikia matatizo yao na kuyatatua.
Sauti ya Mwenyekiti CHADEMA akizungumza
wa upande wao baadhi ya wanachama wa chama cha CHADEMA wakizungumzia kuhusu uchaguzi na maswala ya watu kutekwa, wameiomba serikali kuendelea kufuatilia suala hilo lakini pia kuweka misingi mizuri na usimamizi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.
Sauti ya wajumbe wa chama cha CHADEMA wakieleza namna walivyojipanga kushiriki uchaguzi wa serikali ya mtaa