Mpanda FM

Mbunge Nsimbo akabidhi msaada kwa waathirika wa mafuriko

21 April 2024, 2:09 pm

Mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliopokea misaada hiyo.picha na Ben Dadau

“Wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua ambazo tayari zimeonyesha kuwa na athari ya mafuriko katika jamii”

Na Ben Gadau -Katavi

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amekabidhi msaada kwa wahanga wa mafuriko katika vijiji vya kaburonge A na bulembo kata ya Litapunga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwa wahanga hao Lupembe amewataka wananchi kuendelea kuzingatia matamko mbalimbali ya mamlaka husika ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba zenye uimara ili kuepukana na majanga ya namna hiyo.

Sauti ya mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe akizungumza

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamemshukuru mbunge huyo huku wakiendelea kuiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia wahanga wa mafuriko hayo.

Sauti ya wananchi wakimshukuru mbunge huyo

Mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya kata ya litapunga yametokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 14 mwezi april huku wananchi wakitakiwa kuendelea kuchukua tahadhari .