Mpanda FM

Ukaguzi magari ya shule, onyo latolewa

18 June 2026, 11:55 am

Zoezi la ukaguzi wa magari ya shule likiwa linaendelea, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi aongoza ukaguzi huo. picha na Anna Milanzi

wanafanya ukaguzi huo wakati huu walikizo ili shule zitakapofunguliwa magari hayo yawe yana usalama wa kubeba wanafunzi huku akisema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa ambao watakiuka agizo hilo

Na Anna Milanzi-Katavi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi amewahimiza wamiliki wa mabasi  ya shule mkoani katavi kuyapeleka mabasi  hayo kufanyiwa ukaguzi.

Akizungumza mara baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa mabasi hayo kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Kaster Ngonyani ambaye ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi amesema wamekagua magari 24 na kubaini mapungufu katika magari mawili.

Kamanda Ngonyani amesema wanafanya ukaguzi huo wakati huu walikizo ili shule zitakapofunguliwa magari hayo yawe yana usalama wa kubeba wanafunzi huku akisema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa ambao watakiuka agizo hilo

Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani akizungumza baada ya ukaguzi

Akizungumza kwa niaba ya jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Katavi askari wa jeshi hilo Frank Omwagore amewashauri wamiliki wa magari kuhakikisha magari yao yanakuwa na vizimia moto

Sauti ya askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji Katavi Frank Omwagore akizungumza.

Kwa upande wao madereva na walezi wa wanafunzi katika magari hayo wamepongeza hatua hiyo ya ukaguzi na kuwakumbusha wengine kuzingatia usalama wa watoto.

Sauti ya dereva na mlezi wa watoto kwenye magari wakizungumza kuhusiana na ukaguzi uliofanyika.

Zoezi hilo la ukaguzi linafanyika kwa siku tatu ambapo limeanza june 17, 2026