Mpanda FM

Wanahabari wanolewa kuhusu chanjo ya polio

19 September 2023, 10:06 am

Waandishi wakiwa katika mafunzo ya chanjo ya polio. Picha na Anna Milanzi

Mkoa wa Katavi unatarajia kutoa chanjo kwa Watoto 227,862 ambapo chanjo hiyo itatolewa kwa halmashauri zote tano mkoani hapa.

Na Veronica Mabwile – Katavi
Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kushiriki ipasavyo katika kampeni ya chanjo ya polio inayotarajiwa kuanza kutolewa kuanzia September 21 hadi September 24 mwaka huu kwa lengo la kuwakinga Watoto na ugonjwa huo.

Wameishukuru wizara ya afya kwa kuwapatia elimu juu ya ugonjwa huo ambapo wamesema kuwa watakuwa chachu katika utoaji wa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

Akizungumza mara baada ya kufunga mafunzo ya siku moja yaliyotolewa Kwa waandishi wa Habari juu ya ugonjwa huo Afisa mpango wa taifa kwa huduma za afya ngazi ya jamii wizara ya afya Bahati mwailafu amesema chanjo hiyo itatolewa kwa Watoto wote wenye umri chini ya miaka nane .

Sauti ya Bahati Mwaikafu kutoka Wizara ya Afya

Waandishi wa Habari ambao wameshiriki mafunzo hayo wameishukuru wizara ya afya kwa kuwapatia elimu juu ya ugonjwa huo ambapo wamesema kuwa watakuwa chachu katika utoaji wa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

Sauti ya Waandishi wa Habari walioshiriki mafunzo hayo

Mkoa wa Katavi unatarajia kutoa chanjo kwa Watoto 227,862 ambapo chanjo hiyo itatolewa kwa halmashauri zote tano mkoa hapa.