On air
Play internet radio

Recent posts

31 March 2025, 1:47 pm

amani yasisitizwa katika swala ya eid al fitr

“amani ndio msingi wa maendeleo tuilinde katika mambo yote kama hakuna amani ni ngumu kufanyika chochote ,tuendelee kuiombea nchi yetu amani” Na Samwel Mbugi-Katavi Wananchi mkoani katavi watakiwa kuitunza amani iliyopo kwani ndio jambo lakwanza kabisa kabla ya mambo yote…

27 March 2025, 4:51 pm

Zaidi ya waganga 80 wa tiba asili wapatiwa mafunzo Katavi

Picha ya meneja wa mradi wa VUMA Henry  Bendera. Picha na Restuta Nyondo “Tumebaini vijana wengi hukimbilia kwa waganga kupata matibabu” Na Restuta Nyondo Zaidi ya waganga wa tiba asili 80 kutoka katika wilaya za Mpanda na Tanganyika mkoani Katavi wamepatiwa…

27 March 2025, 4:33 pm

Chadema Katavi wamtemea cheche Makalla

Picha ya Katibu wa CHADEMA wilaya ya  Mpanda Richard Mponeja. Picha na Edda Enock “Msimamo wetu ni kuhakikisha kuwa na uchaguzi huru, wa haki na usalama” Na Edda Enock Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Mpanda mkoani Katavi…

27 March 2025, 3:55 pm

ACT Wazalendo Katavi yawasihi wanawake kugombea nafasi za uongozi

Picha ya katibu wa ACT Wazalendo Katavi. Picha na Anna Mhina “Zaidi ya 75% ni nafasi kwa vijana na wanawake” Na John Benjamin Chama cha ACT wazalendo Mkoa wa Katavi kimewataka wanawake na vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuwania nafasi…

27 March 2025, 3:36 pm

Hofu yatanda kwa wananchi wa Kasimba, chatu mwingine auwawa

Picha ya chatu aliyeuawa. Picha na Anna Mhina “Naomba nitoe rai sitisheni shughuli zote katika mto huo” Na Anna Mhina Wananchi wa mtaa wa Kasimba uliopo kata ya Ilembo wilayani Mpanda mkoani Katavi  wameingiwa hofu baada ya kuuawa kwa nyoka…

26 March 2025, 3:43 pm

Vijana jitokezeni kugombea nafasi za uongozi

“Taifa linahitaji nguvu kazi ya vijana” Na John Benjamin Vijana mkoani Katavi wameombwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali  katika uongozi wa kisiasa Hayo yamezungwa na mwenyekiti wa ngome ya vijana wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi ambapo…

25 March 2025, 9:39 am

Meya Mpanda apiga jeki mifuko 40 ya saruji ofisi za CCM

Wajumbe wa CCM wakipokea mfuko mmoja wa saruji kwa niaba ya mifuko 40. Picha na Anna Mhina “Lengo la kutoa mifuko hiyo ni kukifanya chama kionekane cha tofauti” Na Anna Mhina Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani…

16 March 2025, 3:34 pm

Mfumo wa maombi ya vyeti kwa njia ya kidijitali wazinduliwa rasmi Mpanda

Picha ya Katibu Tawala Wilaya ya Mpanda Jofrey Mwashitete. Picha na John Benjamin “Serikali inaendelea kuimarisha huduma “ Na John Benjamin Wananchi wa wilaya ya Mpanda wameishukuru serikali kupitia ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA kwa kuanzisha…

16 March 2025, 3:25 pm

Wananchi Mpanda walilalamikia jeshi la zimamoto na uokoaji

“Wananchi wanachelewa kutoa taarifa kwa jeshi la zimamoto na uokoaji” Na Anna Mhina Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameliomba jeshi la zimamoto na uokoaji kuweka mifumo bora ili kuweza kufika kwa wakati pindi wanapopokea taarifa za…

16 March 2025, 3:12 pm

Wanawake wajawazito watakiwa kuwahi kuanza kliniki

Picha ya Dkt Gabriel Elias. Picha na Anna Mhina “Ni muhimu kuwahi kliniki ili kuepukana na magonjwa hatarishi yanayojitokeza” Na Edda Enock Wanawake manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kuwahi kuanza  kliniki pale wanapogundua kuwa ni mjamzito ili kupata elimu…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.