Mpanda FM

KKKT wamuaga Ambele Mwaipopo

30 August 2023, 10:07 am

MPANDA

Idara ya wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Jimbo la Katavi wamefanya hafla ya kumuaga Askofu wa Dayosisi ya ziwa Tanganyika Ambele Mwaipopo ambaye anakaribia kumaliza muda wake.

Awali akisoma taarifa Mwenyekiti wa Idara ya wanawake KKKT jimbo la Katavi Felsta Chaula amesema wanawake jimbo hilo watamkabidhi zawadi ya Ng’ombe mwenye thamani ya milioni moja na laki mbili ikiwa ni shukrani ya kuwatumikia kwa muda wote.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuendelea kuliombea taifa .

Kwa upande wake Askofu Ambele Mwaipopo amewashukuru Idara ya wanawake wa KKKT Jimbo la Katavi kwa kuwa wakwanza kufanya tukio la kumuaga.

#mpandaradiofm97.0

#tbconline