Mpanda FM

Wazazi Mkoani Katavi Washauriwa Kuzingatia Matumizi Sahihi ya Dawa kwa Watoto

15 January 2024, 10:28 am

Picha na Mtandao

Dawa hizo Mara nyingi huwa zinatolewa kwa Watoto walio na umri chini ya miaka mitano

Na Gladness Richard-Katavi

Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa maoni mseto juu ya Matumizi sahihi ya dawa za Maji kwa Watoto wenye umri chini ya Miaka 5.

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm Wananchi hao wamesema kuwa kwa kawaida wanatunza dawa  na kuzitumia tena pindi Mtoto anapokuwa amepatwa na Maradhi .

Sauti ya wananchi wakieleza juu ya matumizi ya dawa kwa watoto

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Town Clinic Gabriel Elias Amesema kuwa dawa hizo mara nyingi huwa zinatolewa kwa Watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na amewashauri wazazi kuendeleea kufuata ushauri wa  mtaalamu wa afya.

Sauti ya Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Town Clinic Gabriel Elias

Elias ameongeza kwa kuwaasa Wazazi kuzingatia Matumizi Sahihi ya dawa kwakuwa kutumia dawa ambazo zimeisha muda wake haziwezi kuwa na msaada kwa Mgonjwa.