Mpanda FM

Makatibu CCM Nsimbo wanufaika na pikipiki za Lupembe

9 August 2023, 6:33 am

MPANDA.

Pikipiki kumi na mbili zenye thamani ya shilingi Milioni thelathini zimegawiwa kwa Makatibu kata wa chama cha mapinduzi CCM halmashauri ya Nsimbo na Mbunge wa jimbo hilo Anna Richard Lupembe kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi kwa makatibu hao.

Akizungumza na wananchama wa chama hicho lupembe amesema kuwa lengo la kugawa pikipiki hizo ni kutaka kuimarisha utendaji kazi ndani ya chama cha mapinduzi na kuwarahisishia makatibu kata kuwafikia wanachama kirahisi katika maeneo yao .

Nae mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa katavi Iddi Kimanta amewataka makatibu hao wa kata kuzitunza pikipiki hizo vizuri na zikafanye kazi iliyokusudiwa .

Nao baadhi ya makatibu kata wamesema kuwa kitendo cha Mbunge huyo kugawa pikipiki kwenye kata zote kumi na mbili za halmashauri ya Nsimbo kutawarahisishia kufanya kazi za chama kwa wepesi na haraka huku wakihakikisha ushindi ndani ya chama hicho katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Zoezi hilo la ugawaji wa pikipiki kwa makatibu kata wa Chama Cha Mapindizi CCM umefanyika katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mpanda.

#mpandaradiofm97.0

#ccmtanzania