Mpanda FM

RC Katavi apiga marufuku shughuli katika hifadhi ya barabara

2 December 2023, 3:41 pm

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Wajumbe katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa

hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa Wananchi watakaobainika kufanya Shughuli zilizo kinyume katika hifadhi ya Barabara.

Na Anna Milanzi -Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amepiga marufuku wananchi Wanaolima katika hifadhi ya barabara na kupitisha mifugo kwenye barabara kinyume na utaratibu.

Hayo yamesemwa  katika  kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika November 29, 2023  katika Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi eneo la Ilembo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa

Wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi.Picha na Anna Milanzi

Akitoa taarifa Meneja (TANROADS) mkoa wa Katavi Mhandisi Martini Mwakabende na Meneja ( TARURA) mkoa wa Katavi Mhandisi Innocent Mlay wamebainisha changamoto walizonazo katika utekelezaji wa majukumu yao huku changamoto ya wananchi kulima katika hifadhi ya barabara na kupitisha mifugo katika barabara hizo zikiwakabili.

Meneja (TANROADS) Mkoa wa Katavi Mhandisi Martini Mwakabende Akitoa Taarifa .Picha Anna Milanzi

Sauti ya Meneja (TANROADS) Mkoa wa Katavi Mhandisi Martini Mwakabende na Meneja ( TARURA) Mkoa wa Katavi ,Mhandisi Innocent Mlay.

Wajumbe katika Kikao hicho akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijiji Selemani Kakoso Wameshauri hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa Wananchi watakaobainika kufanya Shughuli zilizo kinyume katika hifadhi ya Barabara.

Sauti ya wajumbe, Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso.

Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini akiwa na Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini.Picha na Anna Milanzi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko  amewataka Wakuu wa Wilaya kusimamia suala hilo ikiwemo pia na wizi wa Taa za Barabarani na kuwataka kuwachukulia hatua za Kisheria Wanaokikuka.