Mpanda FM

Wananchi wafunguka juu ya ukamilishaji dozi ya maralia kwa usahihi

14 September 2023, 11:40 am

Picha na Mtandao

Mgonjwa wa maralia anapaswa kukamilisha dozi ya Malaria ambayo anapatiwa na mtaalamu wa afya Ambapo kutamsaidia kumaliza vimelea vya maambukizi ya maralia

Na John Benjamin – Mpanda

Wananchi halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wametoa maoni namna wanavyoelewa kuhusu ukamilishaji wa dozi ya maralia kwa usahihi.
Wakizungumza na Mpanda redio FM kwa nyakati tofauti baadhi wameonyesha kutokamilisha dozi kwa sababu ya kuonyesha kupona huku wengine wakiwa na elimu ya kukamilisha dozi wakiamini ndiyo kunapeleka kupona ugonjwa wa maralia

Sauti ya baadhi ya wananchi wakieleza maoni yao juu ya kukamilisha dozi ya Malaria

Kwa upande mratibu wa maralia manispaa ya Mpanda mkoani hapa Katavi amesema kuwa mgonjwa wa maralia anapaswa kukamilisha dozi ya maralia ambayo anapatiwa na mtaalamu wa afya Ambapo kumtamsaidia kumaliza vimelea vya maambukizi ya maralia

Sauti ya Anord Fungo Mratibu wa Malaria Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi

Mkoa wa katavi ni Moja ya mikoa ambayo inatajwa kuwa na mambukizi kwa kiwango cha juu cha asilimia 8.