Mpanda FM

Wananchi Katavi watakiwa kuchunguza miili yao kuepukana na magonjwa sugu

8 August 2024, 9:28 am

Picha na Mtandao

“kupima afya ya mwili mara kwa mara kunasaidia kuondoa usugu wa magonjwa kwani kama ukibainika kuwa na ugonjwa unatibiwa katika hatua za awali za ugonjwa”

Na Rachel Ezekia-Katavi

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya mpanda mkoani Katavi wametoa maoni  mseto kuhusiana na umuhimu wa  kuchunguza afya ya miili yao   mara kwa mara ili kufanya shughuli za kimaendeleo kwa ufanisi

Wameyasema hayo walipokuwa wanazungumza na Mpanda Radio FM ambapo wameeleza kuwa  watu wengi wamekuwa hawafanyi hivyo kutokana na hofu endapo wakibainika kuwa na magonjwa.

sauti za wananchi wakitoa maoni yao

Daktari Paulo Lugata  ambaye  pia ni mganga mfawidhi wa hospitali ya manispaa ya Mpanda  ameeleza kuwa  kufanya uchunguzi wa mwili au body chekup  kunasaidia kugundua viashiria vya ugonjwa mapema na kutafutia ufumbuzi .

Sauti daktari akizungumzia umuhimu wa kufanya checkup ya mwili

Katika hatua nyingine daktari lugata amesema wananchi wengi wamekuwa wakifika hospitali mpaka wanapoumwa na sikwenda kwa hiari  kuchunguza miili yao.

sauti ya daktari akizungumzia mwenendo wa wananchi kwenda hospitali hadi wanapoumwa

Ameongeza kuwa  ni rahisi kutibu ugonjwa ukiwa katika hatua za mwanzo kwani magonjwa mengi hayaonyeshi dalili kwa  haraka.