Mpanda FM

Katavi: Maji safi na salama bado kilio Kamlenga

10 July 2023, 10:24 am

KATAVI

Wananchi wa kitongoji cha Kamlenga kijiji cha Sibwesa halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi wameiomba serikali iwasaidie upatikanaji wa maji safi na salama ili kuepukana na magonjwa ya tumbo.

Wakizungumza na Mpanda Radio fm wananchi hao wamesema kuwa wanatembea umbali wa kilomita mbili kufuata maji ambayo si salama kwao huku hata usalama wa maisha yao ukiwa hatarini kutokana na uwepo wa wanyama wakali katika maeneo hayo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Sibwesa halmashauri ya Tanganyika Bwana Deus Masunga amesema kuwa wanategemea kupata maji kutoka katika mradi wa maji Kayenze pindi utakapokamilika.

Akizungumzia suala hilo la upatikanaji wa maji Meneja wa Mamlaka ya Maji RUWASA wilaya ya Tanganyika Bwana Alkram Sabuni amesema kuwa upatikanaji wa maji katika kitongoji cha Kamlenga utatokana na upanuzi wa mradi wa maji wa Kayenze pindi utakapokamilika mwishoni mwa mwezi wa nane.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayamaji