Mpanda FM

Shule ya Makomelo Kupunguza Adha ya Mrundikano Shuleni

17 July 2023, 10:15 am

KATAVI

Adha ya Wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Kitongoji cha Songambele Kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka kutembea Umbali wa Kilomita 9 kupata Elimu shule ya Msingi Itenka inatarajiwa kuisha kuanzia Mwezi Agosti pindi itakapokamilika Shule mpya ya Makomelo.

Akizungumza baada ya Kukagua Mradi wa Ujenzi wa Vyumba 14 vya shule ya , vyumba 2 vya shule ya awali , Jengo la Utawala na Matundu 24 ya Vyoo Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amesema kuwa Wanafunzi wanaosoma shule za Itenka na Tumaini wakitokea Kitongoji cha Songambele wa Darasa la Kwanza hadi la Sita watalazimika Kuhamia shule hiyo pindi itakapokamilika.

Awali akisoma Taarifa ya Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Makomelo Method Justine Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Itenka amesema shilingi Milioni Mia Tano na Nane zimetumika hadi sasa katika ujenzi wa Vyumba 16 vya Madarasa, Jengo la Utawala na Matundu 24 ya Vyoo katika mradi huo.

#mpandaradiofm97.0

#ccm

#WizaraYaElimu

#katavists