Mpanda FM

Vijana Katavi watafuta nyeti za wanawake watajirike

7 May 2024, 5:52 pm

Vijana wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji ambao wanafanya ramli chonganishi na wamekuwa wakiwaagiza vijana hao nyeti za wananwake ili wawape njia za mafanikio.

Na Leah Kamala-Katavi

Jeshi la polisi mkoani Katavi limewakamata watuhumiwa 115 wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu wakiwa na vielelezo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amesema wamewakamata watuhumiwa 17 wakiwa na dawa za kulevya na watuhumiwa 31 wakiwa na mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akithibitisha wamewakamata watuhumiwa 17 wakiwa na dawa za kulevya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akionyesha baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokamatwa. PIcha na Leah Kamala

Aidha wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 27 wakiwa na nyara za serikali vipande 21 vya wanyama pori na wamefanikiwa kuwapeleka watuhumiwa 29 mahakamani waliopatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo mbalimbali.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akithibitisha kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 27 wakiwa na nyara za serikali vipande 21 vya wanyama pori.

Pia kamanda amewaasa vijana wa kiume ambao hawapendi kufanya kazi na badala yake wamekuwa wakitaka kutafuta pesa kwa njia za mkato ambapo wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji ambao wanafanya ramli chonganishi na wamekuwa wakiwaagiza vijana hao nyeti za wananwake ili wawape njia za mafanikio jambo ambalo sio sahihi.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akiwaasa vijana wa kiume ambao hawapendi kufanya kazi na badala yake wamekuwa wakitaka kutafuta pesa kwa njia za mkato.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limetoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu na wasifiche taarifa za kihalifu na wahalifu ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wakati.