Mpanda FM

Tanzia Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Mpanda Method Mtepa afariki dunia

20 September 2023, 5:31 pm

Mwenyekiti CCM Wilaya ya Mpanda Method Mtepa enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Taarifa za msiba huo amezipokea kwa masikitiko makubwa sana na kiongozi wake alikuwa anamfahamu kwamba alikuwa mchapakazi katika utendaji wa kazi.

Na Kalala Robert & Anna Millanzi – Mpanda
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Ccm wilaya ya Mpanda Bw. Method Mtepa amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 19/09/2023 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akizungumza na Mpanda radio fm Katibu wa itikadi na wenezi CCM wilaya ya mpanda amesema kuwa taarifa za msiba huo amezipokea kwa masikitiko makubwa sana na kiongozi wake alikuwa anamfahamu kwamba alikuwa mchapakazi katika utendaji wa kazi.

Sauti ya Katibu wa Itikadi na Wenezi CCM Wilaya Mpanda Elias Mwanisawa

Kwa upande wao wanachama wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya mpanda wamesema kuwa msiba huo ni pigo kwao.

Sauti ya Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi

Ndugu wa marehemu amesema ratiba ya ibada ya kuaga mwili itafanyika siku ya kesho na mazishi yatafanyika nyumbani kwao Sumbawanga katika kijiji cha kasanga .

Sauti ya Andrew Peter ndugu wa marehemu