Mpanda FM

Madiwani Halmashauri ya Mpimbwe wajifunza Biashara ya Hewa ukaa

17 January 2024, 12:48 pm

Utunzaji wa Misitu na upandaji Miti unahusisha biashara ya hewa ukaa .Picha na Mtandao

Wanatarajia kuanza kufanya Biashara hiyo kutokana kuwa  na Maeneo yanayoruhusu kufanya   Biashara ya Hewa ukaa.

Na Betord Benjamini-Katavi

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele Mkoani Katavi  wamefanya ziara wilaya ya Tanganyika kujifunza namna Biashara ya Hewa ukaa inavyofanyika.

Wakizungumza  baada ya kupata elimu ya Biashara ya Hewa ukaa  Mwenyekiti wa halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba na Mkurugenzi Mtendaji wa halmshahuri ya Mpimbwe Shamimu Mwariko  wamesema wanatarajia kuanza kufanya Biashara hiyo kutokana kuwa  na Maeneo yanayoruhusu kufanya   Biashara ya Hewa ukaa.

Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri ya Mpimbwe na Mkurugenzi Mtendaji wa halmshahuri hiyo wakizungumza

Kwa upande wake Afisa Maliasili wilaya ya Tanganyika Bruno Mwaisaka ameainisha faida zilizopatikana kutokana na Biashara ya Hewa ya ukaa na kusema wanatarajiwa kupata Zaidi ya Bilioni 17.

 Sauti ya Afisa Maliasili wilaya ya Tanganyika Bruno Mwaisaka

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  dk Samia Suluhu Hassan ameshatoa Mwongozo kuhusu  Biashara ya Hewa ukaa  na kuwataka Watendaji wa Wilaya ya Mlele kuanza utekelelezaji wa Maagizo na kupitia elimu waliyoipata Tanganyika kuanza  Biashara ya Hewa ukaa

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga akizungumza juu ya elimu waliyoipata