Mpanda FM

Wizi koki za maji Katavi chanzo cha kukosekana huduma ya maji

2 April 2024, 10:23 pm

Picha na Mtandao

Wizi wa koki uliokuwa unafanywa na wahalifu ulichangia kwa kiasi kikubwa kukosekana  kwa maji  katika mtaa wa Mpanda hoteli.

Na Samwel Mbughi-Katavi

Wananchi wa Mtaa wa Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda mkoani  Katavi wametoa Shukrani kwa Serikali baada ya kutatua changamoto ya Maji iliyokuwa inawakabili katika eneo hilo .

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Redio Fm na kuongeza kuwa wizi wa koki uliokuwa unafanywa na wahalifu ulichangia kwa kiasi kikubwa kukosekana  kwa Maji  katika mtaa huo.

Picha na Mtandao

Sauti ya wananchi mtaa wa Mpanda hotel

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Christina Mshani  amesema wameshirikiana kwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na chama kuhakikisha huduma ya Maji inarejeshwa  kwa wakati.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpanda hoteli

Nae Diwani wa kata ya Mpanda hoteli Hamisi Richard Misigalo amebainisha kuwa Serikali  inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha maeneo ambayo  maji hayajafika yanafika kwa wakati .

Sauti ya Diwani Kata ya Mpanda hoteli

Hata hivyo Misigalo ameishukuru Mpanda Radio Fm kwa kuendelea kufuatalia maendeleo ya kata ya Mpanda hoteli, ambapo amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Wananchi ambao huduma ya Maji haijawafikia inawafikia.