Mpanda FM

Wananchi Dilifu wajitokeza kuchangia damu

16 June 2023, 7:20 pm

MPANDA

Wananchi wa kijiji cha Dilifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamejitokeza kuchangia damu katika kuadhimisha siku ya Wachangiaji damu Duniani.

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wananchi hao wamesema kuwa wameamua kutoa damu ili kuweza kuwasaidia wanaohitaji kuongezewa damu kutokana na kuwepo kwa uhitaji wa damu kwa sababu mbalimbali.

Kwa upande wake mratibu wa damu wa manispaa ya Mpanda Fabiola Kauzeni amesema kuwa wameweza kupata unit 20 Katika zoezi lililoendeshwa katika Kijiji cha Dirifu na na amewashukuru wale waliojitotelea kuchangia damu.

Kila ifikapo tarehe 14 mwezi wa 6 inaadhimishwa Siku ya wachangia damu duniani na Mkoani Katavi Maadhimisho hayo yanafanyika sehemu mbalimbali ikiwemo wilayani Mlele ambapo mkuu wa wilaya Majid Mwanga anatarajia kuwa mgeni rasmi huku kauli mbiu ni ‘changia damu,changia mazao ya damu,changia mara kwa mara,okoa maisha’.

#mpandaradiofm97.0

#damusalama

#wizarayaafya