Mpanda FM
Mpanda FM
27 May 2026, 5:09 pm

“Amewataka waumini wa dini ya kiislam kuto kugawanyika kwa misingi ya siasa wala ukabila na udini jambo ambalo ni kinyume na taratibu namiongozo ya dini hiyo.”
Na Samwel Mbugi- Katavi
Waumini wa dini ya kiislamu mkoa wa Katavi wamesisitizwa kuwa na upendo na mshikamano kwa serikali iliyopo madarakani katika nyakati zote ili kudumisha amani iliyopo kwa taifa la Tanzania.
Hayo yamesemwa na Sheikh mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Nassor Kakulukulu wakati wa ibada ya swala ya Eid Al-Adha iliyofanyika viwanja vya shule ya msingi kashato iliyopo manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.
Pia Amewataka waumini wa dini ya kiislamu kutokugawanyika kwa misingi ya siasa wala ukabila na udini jambo ambalo ni kinyume na taratibu na miongozo ya dini hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya ibada kumalizika amewataka wananchi wote kuendelea kutunza amani iliyopo ambapo amesema jambo ambalo litawezesha kila mtu kufanya shughuli zake za maendeleo bila kuwa na hofu yoyote.
Hata hivyo Mrindoko amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa makini na uangalizi wa kutosha kwa watoto hususani wanapotoka kwenda kusherehekea sikuku hiyo ya Eid.