Mpanda FM

Mafuriko yazitenganisha Mpanda, halmashauri ya Nsimbo

16 April 2024, 12:12 am

Barababara ambayo ni kiunganishi cha Manispaa ya Mpanda na halmashauri ya Nsimbo imekatika na kukosesha mawasiliano kati ya maeneo hayo mawili. Picha na Lilian Vicent

Kutopitika kwa barabara hii kutasababisha wanafunzi washindwe kwenda shule na hata wananchi watashindwa kuzifikia huduma muhimu kutokana na kutenganishwa kwa barabara hiyo”

Na Lilian Vicent Katavi

Barabara inayounganisha Manispaa ya Mpanda na  Halmashauri ya Nsimbo Imekatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Mafuriko Mkoani Katavi.

Mmoja wa Wananchi waliojitokeza kuangalia hali hiyo ya uharibifu ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa barabara hiyo ni kiunganishi Muhimu kwani Wanafunzi wanapaswa kuitumia kuelekea Shuleni na hata Wananchi kufuata Mahitaji Mjini.

Sauti ya mmoja wa Wananchi akilalamikia hali hiyo na kuiomba serikali ifanye marekebisho ya barabara hiyo kwa haraka

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Mpanda Hidary Sumry amekiri uwepo wa changamoto hiyo na kusema kuwa Barabara hiyo ni Muhimu kwa Wananchi ambapo amewaomba wakala wa Barabara  TARURA  kwa ngazi ya taifa kuwasaidia marekebisho ya Barabara hiyo kwa haraka

Sauti ya Meya wa Manispaa ya Mpanda Hidary Sumry akizungumza mara baada ya tukio hilo na kuiomba Serikali kuharakisha matengenezo ya barabara hiyo

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ametoa pole kwa Wananchi hao na kuwataka kuchukua tahadhari sambamba na kuhama katika maeneo ya Mabondeni.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumza na Wananchi nakuwataka wahame maeneo ya mabondeni

Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa Kuamkia April 14 imeleta Maafa katika Maeneo mengi Mkoani Katavi ikiwamo uharibifu wa barabara na Wananchi kukosa makazi kutokana na Maji kuingia katika makazi ya watu.