Mpanda FM

Wakazi Dirifu waomba utaratibu kusomewa mapato, matumizi

16 June 2023, 7:22 pm

MPANDA

Wakazi wa kijiji cha Dirifu manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamewataka viongozi wa kijiji hicho kuwa na utaratibu wa kuwasomewa mapato na matumizi ili kuongeza uwajibikaji kwa wananchi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara, wananchi hao wamesema kuwa kumekuwa na ukakasi kwa viongozi wa Kijiji hicho kutosoma mapato na matumizi kwa wakati hali ambayo huzua wasiwasi juu ya fedha za maendeleo zinazovyotumika kwenye kijiji chao.

Mwenyekiti wa kijiji cha Dirifu Geofrey Maiko Mbogo amesema kuwa changamoto ya kutosoma mapato na matumizi kwa wakati inatokana na watendaji wengi katika kijiji hicho kuhamishwa na kuwahakikishia wananchi wanasomewa mapato na matumizi ya kijiji kwa mujibu wa sheria ili kuongeza imani.

Katika mkutano huo afisa mtendaji wa kijiji hicho Evirius Mathayo amewasomea mapato na matumizi wananchi kwa mwaka wa 2022 hadi Mei 2023 yenye thamani ya shilingi milion 11.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayatamisemi

#katavists