Mpanda FM

Jeshi la Polisi Katavi laendeleza msako, 17 watiwa mbaroni

6 December 2023, 9:51 am

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani .Picha na Gladness Richard

Jeshi la polisi limewatia mbaroni watuhumiwa wakiwa na lita  135 na mtambo wa kutengenezea pombe ya Moshi huku watu 17 wakikamatwa wakiwa na pombe haramu ya gongo.

Na Gladness Richard Katavi

Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Linaendelea kufanya Doria na Misako mbalimbali ili kubaini ,kuzuia na kupambana na Uhalifu ambapo limefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa wakiwa  na Mali za Wizi Zilizoibiwa katika  Maeneo Mbalimbali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani amesema kuwa wamefanikiwa kukamata Watuhumiwa 121 kwa Makosa mbalimbali huku kati yao wakijihusisha na Wizi,Uporaji na Uzururaji.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa  wamekamata watuhumiwa wakiwa na lita  135 na Mtambo Mmoja wa kutengenezea Pombe ya Moshi huku watu 17 Wamekamatwa wakiwa na Pombe haramu .

Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Limejipanga vyema katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unasimamiwa ipasavyo kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya usalama katika kipindi hiki chote cha kuelekea kwenye Msimu huu wa Sikukuu.