Mpanda FM

Waumini Katavi waombwa kuwapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalum

10 October 2023, 12:15 pm

Makamu Mkuu Askofu wa kanisa la PCCT Steveni Nyanzira wakati wa zoezi la ugawaji wa chakula kwa wahitaji. Picha na Anna Millanzi.

Waumini wa madhehebu mbalimbali mkoani Katavi wameombwa kuwapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee kwa kuwapa msaada wa mahitaji ya kiubinadamu.

Na Veronica Mabwile – Mpanda
Waumini wa madhehebu mbalimbali manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameombwa kuwapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee kwa kuwapa msaada wa mahitaji ya kiubinadamu ikiwemo chakula ili kuwawezesha kuyamudu maisha.
Wito huo umetolewa na Makamu Mkuu Askofu wa kanisa la PENTEKOST CHIRISTIAN CHURCH TANZANIA [PCCT] Steveni Nyanzira wakati wa zoezi la ugawaji wa chakula kwa wahitaji lilofanyika katika kanisa hilo lilopo mtaa wa Mnazi mmoja kata ya Uwanja wa Ndege na kusema kuwa ili kuwasaidia kuwaondolea msongo wa Mawazo.

Sauti ya Steven Nyanzira

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnazi mmoja Arufani Buteme akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi diwani wa kata ya uwanja wa ndege Maiko Kamande amelishukuru Kanisa hilo na kuiomba jamii kuishi maisha ya kusaidiana

Sauti ya Arufani Buteme

Wanufaika wa msaada huo wamesema kuwa wamekuwa wakitengwa na jamii kutokana na mitazamo tofauti tofauti ikiwemo jamii kuwachukulia kuwa watu wasio sitaili kusaidiwan jambo ambalo lina wafanya kuishi maisha ya dhiki sana

Sauti ya Wanufaika