Mpanda FM

Maafisa maendeleo ya jamii kiungo muhimu utekelezaji dira 2050

31 August 2026, 10:56 am

Kushoto ni kaimu katibu tawala Frolence Chrisant na Afisa maendeleo ya jamii mkoa Anna Shumbi. Picha na Restuta

kuandika barua hakupimi utendaji kazi wako unapimwa kwa matokeo yenye tija kwa wananchi”

Na. Restuta Nyondo

Maafisa maendeleo ya jamii mkoani Katavi wametakiwa kutumia dira ya maendeleo ya taifa 2050 katika kuleta maendeleo na usawa wa kijinsia kuanzia ngazi za chini kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano.

Akizungumza na maafisa hao katika mafunzo ya maeneo yanayogusa maendeleo ya jamii  ili kutekeleza dira hiyo Kaimu katibu tawala mkoa  wa Katavi Frolence Chrisant amesema ili kurahisisha utekelezaji wa dira ya taifa ni lazima wajitoe na kuwa wabunifu ili kuleta chachu kwa jamii.

Anna Shumbi ni mkuu wa kitengo cha maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na kuleta maendeleo kwa usawa bila kujali jinsia.

Nao maafisa maendeleo ya jamii wameeleza namna watakavyoteleza afua zote ili kufikia malengo ya dira ya taifa 2050.