Mpanda FM
Mpanda FM
8 September 2026, 12:44 pm

Na Ben Gadau
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda imekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Akizungumza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Joseph Lwamba, wakati wa ziara ya Kamati hiyo Amesema kamati imeridhishwa na miradi iliyotembelewa, huku akipongeza jitihada zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha inatekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa makubwa ya wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph, ameahidi kuwa Serikali ya wilaya ya mpanda itaendelea kusimamia fedha za miradi zinazoletwa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora na viwangio vinavyotakiwa.
Kamati ya siasa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda imekagua mradi wa ujenzi w kituo cha polisi kata ya kakese kilichogharimu Mil 35, ujenzi wa choo matundu 10 na ujenzi wa bwalo la chakula shule ya msingi kakese Mil 56, Ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi kakese Mil 342, ujenzi wa jengo la huduma za watoto wachanga hospitali ya wilaya Mpanda Mil 660 na ujenzi wa barabara za Tactics manispaa ya Mpanda zaidi ya Bilion 21.