Mpanda FM
Mpanda FM
31 August 2026, 10:14 am

”Tanzania ni salama na inaheshimu uhuru wa kuabudu”
Na Restuta Nyondo
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa serikali itaendelea kuimarisha mahusiano mazuri yaliyojengwa kwa mda mrefu na kanisa Katoliki na madhehebu yote nchini ili kuleta maendeleo.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 jimbo Katoliki Mpanda yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari St.Mary iliyopo manspaa ya Mpanda amepongeza jimbo hilo kwa kuendelea kuchangia kukuza sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu.
Aidha Waziri mkuu amechangia kiasi cha shilingi milioni 50 kwaajili ya ujenzi wa jengo la ofisi ya jimbo katoliki Mpanda na ukumbi ambao unatarajiwa kupewa jina la muasisi wa jimbo hilo.
Kwa upande wake Askofu wa jimbo Katoliki Mpanda Esebius Nzigirwa amesema kuwa katika miaka 25 wanaendelea kusambaza huduma ya kitume na kuwashukuru wakuu wa majimbo Jirani walioshiriki katika kufanikisha huduma hiyo kutokana na changamoto ya uhaba wa mapadre na kumshukuru Waziri mkuu kwa kufika na kuchangia ujenzi.
Nao waumini wa kanisa hilo wamesema kuwa wanajivunia mafanikio mbalimbali katika jimbo lao na wataendelea kulinda maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali ili kutangaza injili.
Jimbo Katoliki la Mpanda lilianza mwaka 2001 likianzishwa chini ya hayati askofu Paschal William Kikoti