Mpanda FM

Kutotekelezwa kwa sheria ya misitu kunavyochochea ukataji holela wa misitu Katavi (sehemu ya pili)

11 September 2026, 10:29 am

ofisi ya mtendaji Sitalike. Picha na Restuta Nyondo

kuna miradi mingi tunaibaini inakiuka masharti ya vyeti tunavyotoa”

Na Restuta Nyondo

Karibu kusikiliza sehemu ya pili ya makala inayoangazia utekelezaji kifungu cha sheria ya misitu 20002 na kifungu cha 81 cha sheria ya usimamizi wa mazingira 2004 kunasababisha ukataji holela wa misitu na kuharibika kwa mapitio ya wanyamapori kutokana na upanuzi wa eneo la uwekezaji KMCL hali iliyosababisha migogoro kati ya binadamu na wanyamapori na uharibifu wa vyanzo vya maji mkoani Katavi.

Makala hii imezungumza na meneja wa kanda ya magharibi kutoka baraza lauhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC  Edger Mgila ambapo amesema hakuna mradi wowote unaoruhusiwa kuanzishwa kabla haujapewa cheti cha utunzaji wa mazingira.

Aidha ameutaja mkoa wa Katavi kama eneo ambalo limeanza kuharibu mazingira kwa kasi hususani uchimbaji wa madini kwenye vyanzo vya maji.