Mpanda FM

Vicoba kutumika katika uhifadhi wa mazingira Katavi

1 October 2026, 4:30 pm

Wanufaika wakipokea hundi mradi wa Nature Fundi. Picha na Almasi

“Kuna siku 2 katika wiki ni marufuku kuingia msitu wa kijiji“

Na. Restuta Nyondo

Zaidi ya vikundi 32 vya wakulima vya kuweka na kukopa fedha vimenufaika kupitia mradi wa NATURE FUNDI unaolenga kusaidia katika kukuza  uzalishaji na utunzaji wa mazingira mkoani Katavi.

Akizungumza katika kikao cha kukabidhi hundi ya shilingi milioni 38 mgeni rasmi  ambaye ni katibu tawala anayeshughulikia Uchumi na uzalishaji mkoa wa Katavi Nehemia James amewataka wataalamu wa serikali kusimamia katika maeneo yanayonufaika ili kuleta matokeo chanya  ya utunzaji wa mazingira na kilimo endelevu.

Sauti ya Katibu tawala msaidizi

Baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameiambia mpanda radio kuwa kupitia mradi huo wamefanikiwa kukuza Uchumi wa vikundi vyao na kuhamasisha jamii kutunza mazingira ikiwemo kutengeneza sheria ndogo za vijiji zinazosaidia kuzuia shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa vyanzo vya maji.

Sauti ya wanavikundi vya uhifadhi

Shukuru Tweve ni mratibu wa miradi katika taasisi ya Rikolto amesema kuwa wamefanikiwa kufikia asilimia 75 ya utekelezaji ya mradi mpaka sasa kwa kufikia vikundi 85 kati ya 100 na wakulima 3950 kati ya 5000 waliokua wanalenga kuwafikia hadi ifikapo 2027.

Sauti ya mratibu wa mradi

Mradi wa NATURE FUNDI unatekelezwa kwa mwaka 2024/2027 na Rikolto kwa kushirikiana na Timap unatekelezwa katika mikoa ya Katavi,Songwe na Mbeya.