Mpanda FM

Madiwani na watendaji toeni elimu mpango wa bima ya afya kwa wote

24 November 2026, 12:20 pm

Baadhi ya wanaufaika wa bima ya afya kwa wote wakiwa na vitambulisho vyao. Picha na Saga Mwigulu

“Bima ya afya kwa wote ina gharimu kiasi cha 150,000 kwa kaya ya watu 6“

Na. Ben Gadau

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imezindua rasmi zoezi la uandikishaji wa wananchi katika mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa urahisi.

Akizungumza katika uzinduzi wa zoezi hilo, mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph, Lyoba Shomari Juma, amewataka madiwani pamoja na watendaji wa vijiji na mitaa kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango huo ili waweze kunufaika na huduma za afya kupitia bima hiyo.

Sauti ya Lyoba Shomari

Kwa upande wake, Mratibu wa Bima ya Afya kwa Wote kutoka (NHIF), Mkoa wa Katavi, Mohamed Katoto, amesema kuwa bima hiyo inagharimu shilingi 150,000 kwa mwaka na inatoa fursa kwa kaya moja yenye jumla ya watu sita (6) kupata huduma za afya kupitia mpango huo.

Sauti ya mratibu wa bima

Kwa upande mwingine wananchi wamshauriwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo, ili kutumia fursa hiyo kujiunga na mpango wa Bima ya Afya kwa Wote na kuhakikisha wanakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu.

Mgeni rasmi akimkabidhi mmoja ya wanafuaika bima ya afya kwa wote. Picha na Saga Mwigulu