Mpanda FM
Mpanda FM
7 October 2026, 5:28 pm

“mwanzo ilikua inachukua tani 665 kwasasa tumefikia tani 28,279“
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amepongeza utendaji kazi wa bandari ya Karema, akisema maboresho ya miundombinu yaliyofanywa na Serikali yameongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia shughuli za biashara na usafirishaji, ikiwemo kutoka na kwenda nchi jirani.
Mrindoko atoa pongezi, wakati wa ziara yake katika bandari hiyo, ambapo amesisitiza kuwa uwekezaji katika miundombinu umeifanya Karema kuwa sehemu muhimu ya kuchochea biashara na uchumi wa Mkoa wa Katavi.
Aidha amewataka watendaji wa bandari ya Karema kuendelea kutoa huduma kwa weledi, ufanisi na kuzingatia viwango vinavyokidhi mahitaji ya watumiaji, ili fursa zinazotokana na maboresho ya miundombinu zitumike kikamilifu.