Mpanda FM
Mpanda FM
25 November 2026, 4:50 pm

“Wilaya ya Tanganyika ni miongoni mwa ameneo yanayopakana na nchi jirani kama Congo kupitia ziwa Tanganyika“
Na. Mwandishi wetu
Ujumbe kutoka idara ya uhamiaji Dar es Salaam makao makuu ya jeshi la polisi kupitia divisheni ya polisi jamii na shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM), umetoa elimu ya usalama wa binadamu, kutambua na kuzuia makosa yanayovuka mipaka pamoja na kuimarisha ushirikishwaji wa jamii katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Ujumbe huo unaongozwa na ASI Kijanah Msengi kutoka Idara ya Uhamiaji, akishirikiana na ASP Athuman Sultan na Insp. Tamimu A. Mbegu kutoka Makao Makuu ya Polisi, Divisheni ya Polisi Jamii, pamoja na Seira Kepha, Afisa Miradi kutoka IOM.
Akizungumza na ujumbe huo, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usalama wa binadamu na nafasi yao katika kuzuia vitendo vya uhalifu, hususan katika maeneo ya mipakani.
Katika ziara hiyo, ujumbe utafanya mafunzo ya siku tatu kwa maafisa wa Serikali na viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, kabla ya kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la mpakani Ikola, kwa lengo la kuongeza uelewa na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya usalama.
