Mpanda FM

Mafundisho ya dini suluhu migogoro ya ndoa

30 October 2026, 12:35 pm

Shekhe Othman Ramadhan akiwa studio za Mpanda radio Fm. Picha na Leah Kamala

“kila mwanandoa anapaswa kuheshimu misingi ya upendo na haki za mwenzake“

Na. Leah Kamala

Baadhi ya wanandoa mkoani Katavi wameeleza namna wanavyotumia mafundisho ya dini kama msingi wa kujenga maelewano katika familia zao.

Wakizungumza na mpanda radio fm, wanandoa hao wamesema kuwa mafundisho ya dini wanayoyapata katika nyumba za ibada yamewasaidia kutambua umuhimu wa kutanguliza amani na kuelewana katika familia.

Sauti ya baadhi ya wanandoa

Kwa upande wao viongozi wa dini akiwemo Mchungaji Simon Meleka pamoja na Shekhe Othman Ramadhan, wamesema kuwa wanandoa wanahitaji upendo wa dhati, ushirikiano huku kila mmoja akitimiza wajibu wake na kuheshimu haki za mwenzake.

Sauti viongozi wa dini

Aidha wanandoa wameshauriwa kufuata misingi ya ndoa na kujadili masuala yanayohusu familia pamoja na kumtanguliza Mungu.

Sauti ya viongozi wa dini 2