Mpanda FM
Mpanda FM
19 October 2026, 10:14 am

“kama wanataka tulipe ushuru basi tukubaliane na hiyo pesa tutakayolipia ije mja moja kuboresha miundombinu ya soko“
Na. Leah Kamala
Wafanyabiashara na wajasiriamali wa soko jipya mtaa wa kilimani kata ya Nsemulwa Manispaa Mpanda wametakiwa kuotoa ushuru wa soko ili kuboreshewa miundombinu ya soko .
Hayo yamesemwa na mkuu wa idara ya viwanda na biashara Paul Kaoya na kuwataka wajasiriamali hao kupokea mabadiliko kwaajili ya maendeleo ya soko.
Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wameiomba serikali kuwaruhusu kufanya biashara pasipo kutoa ushuru kwakuwa miundombinu bado haijafanyiwa marekebisho.
Aidha Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilimani Frolence Mbambule ameiomba serikali kutoa muongozo sahihi ya maboresho ya miundombinu hiyo ili kupunguza lawama zinazojitokeza kutoka kwa wafanyabishara.
Hata hivyo diwani wa kata Nsemuliwa Alex Ngereza amesema kuwa ni vyema kuwaelimisha wananchi sehemu sahihi ya kufanyia biashara na kuwatengenezea barabara wananchi wa soko hilo.