Mpanda FM

Wanawake wapeta pumba Mpanda waomba kukumbukwa fursa za mikopo

20 November 2026, 3:56 pm

Eneo la Mpanda hotel viwandani lilio na pumba za mpunga . Picha na Leah Kamala

“kazi hii inatusaidia kujikimu katika maisha na kutunza familia zetu“

Baadhi ya wanawake wanaojishughulisha na shughuli za kupeta pumba wamehimizwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ili kujitegemea na kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza na mpanda radio fm, wanawake hao wamesema kuwa kujishughulisha na kazi halali kumeweza kuwasaidia kugharamia mahitaji yao ya kila siku pamoja na kuchangia maendeleo ya familia zao

Sauti za wanawake

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi Kasara Burema ameeleza namna fursa za kiuchumi zinavyoweza kuwasaidia wanawake ili waweze kukuza shughuli zao na kuongeza kipato.

Sauti ya afisa maendeleo

Wanawake wanaojishughulisha na upetaji wa pumba wanapaswa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali pamoja na kupata elimu ya ujasiriamali ili waweze kuboresha maisha yao