Mpanda FM

Mama akata nyeti za kichanga cha siku 4 Mpanda

30 October 2026, 12:22 pm

Picha ya kisu. Picha kutoka mtandaoni

“uchunguzi wa awali umedai kuwa mama anatatizo la afya akili“

Na. Betord Chove

Jeshi la polisi mkoa wa Katavi  Linamshikilia mwanamke  jina limehifadhiwa mkazi wa kijiji  cha Kapalala kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata nyeti mtoto wake mchanga wa jinsia ya kiume mwenye siku nne tangu kuzaliwa.

Tukio hilo limetokea October 25 majira ya saa tatu asubuhi wakati bibi yake alipokua anamuogesha ndipo alipogundua kuwa sehemu zake za siri zimekatwa.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa  mtuhumiwa kuwa na tatizo la afya ya akili na mtoto anaendelea  kupatiwa matibabu katika  hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi inaendelea vizuri.

Jeshi la polisi mkoa wa Katavi linatoa wito kwa baadhi ya wazazi na walezi kuacha mara moja  tabia ya kuwafanyia  watoto vitendo vya unynyasaji na ukatili.